- Tangazo -
Home Uvumbuzi Jukwaa la wanasayansi vijana kuchagiza ubunifu Africa

Jukwaa la wanasayansi vijana kuchagiza ubunifu Africa

- Tangazo -

Arusha. Jukwaa la wanasayansi vijana limeanzishwa ili kuendeleza ubunifu wa kisayansi na kiteknolojia na kuhimiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

STEMi-Africa imeanzishwa na wanasayansi vijana pamoja na wanafunzi kutoka nchi 12 za Afrika na itafanya kazi chini ya ulezi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

“Ndoto yake kuu ni kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika masomo yanayohusiana na sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu (STEM) katika shule na vyuo “, amesema rais wa jukwaa hilo Bi Grantina Moderm.

Pia jukwaa hilo litafanya kazi kama kituo cha kufundishia wanasayansi, wahandisi na wabunifu vijana ambao wataongeza msukumo katika sayansi na teknolojia katika nchi zao husika.

Bi Moderm  ameyasema hayo wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako aliponzidua jukwaa hilo katika kampasi ya NM-AIST, jijini Arusha.

STEMi-Africa itaunga mkono programu nyingine za maendeleo za kimataifa na barani Afrika kama vile malengo endelevu ya kimaendeleo ya Umoja wa Mataifa na Ajenda ya Afrika ya Mwaka 2063.

Ajenda hiyo inalenga kuona Afrika iliyositawi ifikapo mwaka 2063 ikiegemea zaidi ukuaji jumuishi ambao utakuza, pamoja na mambo mengine, pato la kila mtu theluthi tatu zaidi kuliko viwango vya mwaka 2013.

Fursa za kazi zitakuwepo kwa angalau mtu mmoja kati ya watu wanne wanaotafuta kazi na saba kati ya 10 kwa wahitimu Afrika waliokosa elimu ya juu na kupata elemu ya mafunzo ya ufundi.

Kama itatekelezwa vizuri kupitia msaada wa watunga sera, ajenda ya Afrika ya Mwaka 2063 inatarajia pato la ndani la Taifa kwa nchi za Afrika litakua kwa asilimia saba ifikapo mwaka 2063.

Akizindua jukwaa hilo, Prof. Ndalichako aliwapa changamoto jamii ya wanasayansi kubuni vyanzo mbadala vya kupata fedha kwa ajili ya taratibu za programu zao ili kupunguza utegemezi kutoka mfuko wa Serikali.

“Ni vigumu kutatua mahitaji yote ya kila mwanasayansi na kwa kila taasisi “, alisema waziri, na kuongeza pamoja na majukumu muhimu yaliyokuwa sawa na vikwazo vya kifedha, Serikali haitaweza kupata fedha kwa ajili ya miradi yote ya kiutafiti.

Prof. Ndalichako alitambua mchango wa wanasayansi wanawake katika kutatua matatizo yanayokabili jumuiya za ndani kupia tafiti.

Hata hivyo, alisema pamoja na majukumu hayo ya kusaidia programu za tafiti za kisayansi, Serikali inaupungufu wa fedha kuhudumia mahitaji ya wanasayansi wanawake na makundi mengine.

“Pia tunatarajia wanasayansi watapata fedha kutokana na mipango yao wenyewe ili kuendeleza kazi zao za kiutafiti,” alisisitiza, akiihimiza jukwaa hilo kutumia programu za STEM zilizoanzishwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Balozi wa Jukwaa la Next Einstein (NEF)Tanzania Dkt Lwidiko Edward, aliahidi kusaidia mpango huo kupitia Wiki ya Sayansi ya Afrika inayofanyika kila mwaka.

NEF inaangazia wabunifu wa Afrika na kuweka msukumo wa ushirikiano wa kisayansi kwa ajili ya maendeleo ya binadamu.

- Tangazo -
MwanaSayansi
MwanaSayansihttps://sayansi.medicopress.mediai
MwanaSayansi ni chanzo mahususi cha habari, maoni na uchambuzi kuhusu sayansi na teknolojia nchini Tanzania; hasa katika nyanja ya maendeleo. Taarifa zote na maudhui huzingatia sera na taratibu za MedicoPRESS, asasi iliyoanzishwa kwa lengo la kukuza ujuzi wa waandishi wa habari na wanasayansi katika kuwasilisha taarifa za kitabibu na kisayansi kwa jamii kupitia vyombo vya habari.
- Tangazo -

Tufuate

570FansLike
330FollowersFollow
100SubscribersSubscribe

Makala Mpya

- Tangazo -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Tangazo -