- Tangazo -
Home Mazingira Kuna upotevu wa bioanuai katika mlima Kilimanjaro

Kuna upotevu wa bioanuai katika mlima Kilimanjaro

- Tangazo -

[Dar es Salaam] Kuna upotevu wa bioanuai (viumbe hai na mazingira yake) katika sehemu za nchi kavu ya milima ya tropiki kutokana na shughuli za kibinadamu hususani kilimo pamoja na mabadiliko ya tabia nchi. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa katika Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na wataalamu 50, athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na shughuli za kibinadamu katika maeneo ya milimani, si jambo linalofahamika sana na kutiliwa mkazo na mamlaka pamoja na jamii kwa ujumla.

Watu wanaoishi katika maeneo hayo ya milima hutegemea bioanuai kwaajili ya kuendesha maisha yao na hicho ndicho kimewasukuma wanasayansi hao kufanya utafiti juu ya viumbe hai na mazingira yao katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania.

“Takwimu zetu zinaonyesha kuwa athari kubwa zaidi iko katika maeneo ya tambarare na sehemu za milimani zenye ubaridi,’’ utafiti huo uilochapishwa katika jarida la Nature (March 27), umesema.

“Utafiti wetu unaonyesha kuwa matumizi ya ardhi katika sehemu za milimani yanachangia katika kupunguza uwezo wa mazingira katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi,’’ watafiti wanasema.

Mtafiti mkuu, Marcell Peters, kutoka katika Idara ya Ekolojia ya wanyama na baiolojia ya Kitropiki-chuo kikuu cha Würzburg, Ujerumani, amemwambia MwanaSayansi, kuwa matumizi ya ardhi yanaathiri michakato ya ikolojia hasa katika ukanda wenye joto kali na nchi kavu uliopo chini kabisa ya Mlima Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Peters, tatizo hilo limechagizwa zaidi na wakazi wa maeneo hayo kuvuna mazao bila kuwa na kipimo, kupanua maeneo ya kilimo huku wakipunguza uoto wa asili na miti inayoota pembeni mwa milima.

“Ili kutunza udongo, mimea na wanyama muhimu, inabidi wakulima waanze kutumia mbinu za kilimo ambazo haziathiri michakato ya ikolojia. Watumie mbinu zinazoweza kutunza mazingira kwa uendelevu,’’ ameshauri.

“Muda unavyokwenda, hii inaweza kuongeza mapato zaidi kuliko kilimo cha mashamba makubwa,’’ aliongeza.

Kwakutumia maeneo 60 yakitafiti yaliyowekwa latika miinuko; kuanzia chini kwenda juu kusini mwa mlima Kilimanjaro, watafiti hao walifanya vipimo mara kadhaa na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mimea, wadudu, ndege na viumbe wa kundi la mamalia. Walikusanya takwimu kuanzia Januari 2011 hadi Disemba 2016.

Ni jamii chache ya viumbe hai walipotea katikati ya miinuko ya milima ambapo kuna theluji lakini pia penye joto kiasi. Katika maenoe hayo, wakazi hupendelea kulima kahawa na ndizi kwa kutumia mbinu za jadi, alielezea Peters.

Hatahivyo, watafiti hao walitambua athari kubwa katika ukanda wenye joto kali na ukavu wa savanna sehemu ya chini ya Mlima Kilimanjaro ambapo wakazi hupendelea kulima mahindi.

Wanasayansi hao wanasema kwamba takwimu zilozopatikana katika utafiti huo zinaweza kutumika katika kutekeleza mipango endelevu ya kulinda mazingira katika Mlima Kilimanjaro.

Padili James, mtaalamu wa mazingira na mwana jiografia kutoka Tanzania, anasema kwamba utafiti huu umekuja muda mwafaka ambapo kuna uhitaji mkubwa wa chakula katika maeneo mengi ambayo yako karibu na Mlima Kilimanjaro, hivyo kupelekea shughuli za kilimo kuwa nyingi katika ukanda huo,

“Katika kuzungumza na wakazi wa Moshi, sehemu jirani kabisa na mlima Kilimanjaro, nimetambua kuwa shughuli za kilimo ni chanzo kikubwa cha upotevu wa viumbe hai katika maeneo ya chini ya mlima,’’ anasema Padili.

- Tangazo -
MwanaSayansi
MwanaSayansihttps://sayansi.medicopress.mediai
MwanaSayansi ni chanzo mahususi cha habari, maoni na uchambuzi kuhusu sayansi na teknolojia nchini Tanzania; hasa katika nyanja ya maendeleo. Taarifa zote na maudhui huzingatia sera na taratibu za MedicoPRESS, asasi iliyoanzishwa kwa lengo la kukuza ujuzi wa waandishi wa habari na wanasayansi katika kuwasilisha taarifa za kitabibu na kisayansi kwa jamii kupitia vyombo vya habari.
- Tangazo -

Tufuate

570FansLike
330FollowersFollow
100SubscribersSubscribe

Makala Mpya

- Tangazo -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Tangazo -