- Tangazo -
Home Maoni ya MwanaSayansi Vinasaba huamua namna mwili wako unavyofanya kazi

Vinasaba huamua namna mwili wako unavyofanya kazi

- Tangazo -

Je umeshawahi kujiuliza ni kitu gani hufanya wewe kuwa na ufanano wa wazazi wako? Umewahi kujiuliza ni kwa kiasi gani unafahamu kuhusu mlolongo wa uzao kwenye familia yenu? Je kuna matatizo ya kiafya yanayotembea ndani ya familia kutoka kizazi hadi kizazi? Ni matatizo gani ambayo babu yako au baba yako anayo? Je itakuwaje kama haya matatizo yatawakumba watoto wako kupitia wewe?

Sayansi ya vinasaba huwa na majibu kuhusu maswali haya yote. Sayansi kuhusu vinasaba hutupatia nyenzo zinazotusaidia kung’amua majibu kwa namna gani baadhi ya magonjwa na vihatarishi vyake huweza kurithishwa kutoka uzao mmoja hadi uzao mwingine.

Ili kuelewa namna ambavyo vinasaba hufanya kazi ni muhimu tupate ufahamu kuhusu kitu kinachoitwa ‘Genome”. Genome ni kama muunganiko wa maagizo yote ambayo huongoza jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi na namna gani muonekano wetu wa nje unatakiwa kuwa.

Katika mwili vinasaba huwa kama viungo vya vyakula katika kitabu cha mapishi. Baadhi ya vinasaba hufanya mtu awe na nywele zilizojiviringa, awe na macho ya rangi ya kahawia. Pia vinasaba vingine hutusaidia kuongoza namna mwili unavyotumia vyakula na utendaji kazi wote wa mwili kila siku.

Vinasaba hupangwa kwa ustadi mkubwa na kutengeneza mfuatano mithiri ya nyuzi ambazo huitwa kromosomu. Katika kila seli hai ndani ya binadamu kuna jumla ya kromosomu 46 zinazopatikana ndani, kromosomu hizi huwa katika jozi 23. Jozi hizi 23 hutilia ndani jozi mbili za jinsi ambazo ni kromosomu X na Y.

Dondoo ambazo ni lazima kuzifahamu

Binadamu tunafanana chembe za DNA kwa zaidi ya asilimia 99.9. Tunatofautiana asilimia 0.1 tu

Mambo yanapokwenda ndivyo sivyo

Kuna wakati hutokea makosa kwenye vinasaba. Makosa haya ya kijenetiki ni sawa na makosa ya kwenye kitabu cha mapishi kama tulivyozungumza nyuma. Katika kitabu cha mapishi ukiwa na kiungo kilichokosewa, pishi huwa bovu. Makosa ya kijenetiki yanaweza kutokea katika namna mbili. Namna ya kwanza ni kurithi moja kwa kutoka kwa wazazi. Namna ya pili ni kupitia visababishi vya kimazingira kama vile kupitia mionzi ya jua aina ya UV na sababu nyingine zaidi. Kumbuka, vinasaba vikifanya kazi vyema na mwili pia hufanya kazi vyema

Magonjwa yanayosababishwa na hitilafu za kijenetiki

Magonjwa ya kijetiki hutokea kwa namna mbalimbali. Kuna magonjwa ambayo hutokea kwa sababu ya hitilafu kwenye kinasaba kimoja. Mfano wa magonjwa haya ni ugonjwa wa siko seli, ugonjwa wa huntigton, upofu wa kuona rangi nk. Magonjwa mengine husababishwa na hitilafu kwenye vinasaba vingi zaidi ya kimoja. Mfano wa magonjwa haya ni amoja na ugonjwa wa moyo, ugonwa wa Alzheimer, ugonjwa wa Parkinson, kisukari nakadharika. Magonjwa mengine husababishwa na hitilafu za kromosomu kama ugonjwa wa Down, ugonjwa wa Turner, Ugonjwa wa Cri du chat nk.

Upimaji wa vinasaba mapema

Upimaji vinasaba unaweza kutumika kugundua kama mwanamke ana vinasaba vyenye hitilafu ambayo husababisha saratani ya matiti. Matokeo ya upimaji huu hutoa nafasi ya mapema kwa hatua za kimatibabu za haraka kuwai saratani kabla haijatokea na kusambaa.

Kwa nyongeza; upimaji wa vinasaba huweza kugundua kasoro za kijenetiki hata kwa mtoto aliye tumboni hajazaliwa. Kwa sasa kuna zaidi ya vipimo vya kijenetiki zaidi ya 1000; kadri siku zinavyoenda vipimo vingi vinazidi kuvumbuliwa.

“Upimaji wa vinasaba ni jambo la hiari, hii ni kutokana na faida zake na kutilia ndani changamoto zake. Kwa kawaida kuna mtaalamu wa ushauri wa kijenetiki ambaye anaweza kusaidia kutoa elimu kuhusu upimaji wa kijenetiki. Pia hutoa taarifa kuhusu faida na hasara za upimaji vinasaba. Mtaalamu wa ushauri wa kijenetiki pia atakusaidia kujadiliana kuhusu upimaji na athari zake kiakili na kijamii” Hii ni kutoka tovuti rejea ya Genetic Home Reference.

Upimaji wa vinasaba unaweza kufanywa kupitia damu, mate, uboho wa mfupa, tishu za misuli, majimaji ya amnioni na tishu nyingine zote.

Gharama za upimaji wa vinasaba huwa kati ya dola za kimarekani 100 hadi 5,000 kutegemea na aina ya kipimo kinachofanyika.

Sayansi ya vinasaba hasa matumizi ya upimaji wa vinasaba yanafungua njia kwenye uwanda wa matibabu; hii inatoa tumaini la kuboreshwa kwa uchunguzi na matibabu.

Makala ya mwanzao iliandaliwa na Zahir Alimohammed. Imetafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili na Dkt Norman Jonas.

- Tangazo -
Avatar
Mohamed Zahirhttp://tshg.or.tz/about-us/
Mohamed Zahir Alimohamed is a trained Molecular Biologist and Biotechnologist. He is currently pursuing a PhD in medical genetics in The Netherlands and Tanzania, studying the use of next generation sequencing in clinical diagnostics of genetic disorders. He is currently a board member of the African Society of Human Genetics, eLife community ambassador 2019 (representing Africa and Europe) and a co-founder and interim secretary general of the Tanzania Society of Human Genetics.
- Tangazo -

Tufuate

570FansLike
330FollowersFollow
100SubscribersSubscribe

Makala Mpya

- Tangazo -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Tangazo -