Katika nyakati hizi ambazo mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (uliopewa jina la COVID-19) unazidi kuleta wasiwasi miongoni mwa jamii duniani kote, ni muhimu kuzingatia taarifa zenye ukweli wa kisayansi kuhusu virusi hivyo na njia sahihi za kujikinga dhidi ya maambukizi. Hadi sasa, zaidi ya watu 100,000 duniani kote wameambukizwa. Wataalamu wa afya wana nafasi muhimu sana, hususani katika kusaidia jamii kukabiliana na maambukizi ya virusi hivi.
Katika mahojiano haya kati ya MwanaSayansi na Dkt Grace Saguti wa Shirika la Afya Duniani(WHO)-ofisi za Tanzania, jamii ya watanzania inapewa ujumbe kuhusu mambo ambayo wataalamu wa afya wanapaswa kuielekeza jamii endapo kutatokea mlipuko wa ugonjwa huu, licha ya kwamba mpaka sasa Tanzania hakuna kisa cha mgonjwa mwenye virusi hivyo kilichothibitishwa na mamlaka za afya. Fuatilia mahojiano:
MwanaSayansi: Kuna uhitaji mkubwa wa taarifa sahihi kuhusu ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona. Je ni taarifa gani muhimu wataalamu wa afya nchini Tanzania wanatakiwa kuzifikisha kwenye jamii kuhusu ugonjwa huu na kwanini hizi taaria zitolewe?
Dkt Saguti:Taarifa muhimu ambazo wataalamu wa afya wanatakiwa kuwafikishia watanzania na jamii kwa ujumla kuhusu ugonjwa wa COVID19, ni pamoja na kujikinga na maambukizi iwapo itatokea kuna mtu ana dalili za ugonjwa huu nchini.
Hatua hizi ni muhimu:
- Osha mikono yako kwa maji na sabuni au kwa kutumia kimiminika maalum cha kusafishia mikono pia usishikeshike macho, pua au mdomo iwapo mikono yako ni michafu.
Kwa nini? Unaposafisha mikono kwa maji na sabuni unaondoa virusi kwenye mikono.
- Jiweke mbali kidogo (walau mita 1) na watu wanaokohoa , kupiga chafya na wana homa.
Kwa nini? Kwa sababu mtu mwenye maambukizi ya COVID19 anapokohoa au kupiga chafya hurusha mate ambayo huwa na virusi. Kama upo karibu yake unaweza kuvuta virusi kwa njia yako ya hewa.
- Jidhibiti kushikashika macho, pua na mdomo
Kwa nini? Mikono hugusa sehemu nyingi sana, sehemu nyingine huweza kuwa na virusi. Iwapo utagusa macho yako au pua au mdomo na mikono yenye virusi utapata maambukizi.
- Iwapo una homa, mafua , shida kwenye kupumua tafuta msaada wa yiba haraka. Kama uliwahi safiri kwenda China hivi karibuni au umewahi kukutana na mtu ambaye alisafiri kutokea China na ana dalili za mafua mwambie tabibu wako.
Kwa nini? Unapokuwa na dalili za homa, mafua na kikohozi ni muhimu kwenda kituo cha afya au hospitali maana hiyo yaweza kuwa ni kwa sababu ya maambukizi kwenye njia ya hewa au ugonjwa mwingine hatari zaidi. Dalili hizi huwa na sababu nyingi na kutegemea na hali au historia ya kusafiri virusi vya corona huweza kuwa sababu mojawapo.
MwanaSayansi: Je, ni jambo gani unadhani jamii ya Watanzania hawafahamu na wanapaswa kuelezwa katika kipindi hiki ambapo kuna huu ugonjwa kwenye nchi mbalimbali duniani?
Dkt Saguti: Wajue kuwa dunia iliwahi kukumbwa na mlipuko wa aina nyingine ya virusi vya corona iliyoitwa SARS. Mlipuko wa SARS ulitupa uzoefu kwenye kufanya maandalizi na kupeana taarifa kuhusu milipuko ya magonjwa. Dunia imepiga hatua katika kufanya tafiti, hivyo watu duniani kote wawe na imani kuwa ugonjwa huu wa COVID-19 utadhibitiwa kama ilivyokuwa kwa virusi vya corona aina ya SARS miaka 17 iliyopita . Kirusi hiki kipya cha corona kinasambaa haraka na kinatumia muda mrefu kuzaliana bila kuonyesha dalili, hii ni moja ya changamoto katika kudhibiti hiki kirusi
Japokuwa kuna ogezeko wagonjwa wenye COVID-19 kila siku, wananchi hawatakiwi kuwa na hofu sana ila wanatakiwa kujifunza na kuzielewa kanuni za usafi binafsi. Kama unahisi mafua na una homa, epuka kwenda kwenye mikusanyiko ya watu na muone daktari haraka. Mamlaka za afya zinafanya kazi kujijengea uwezo wa kuchunguza maambukizi hasa kwenye viwanja vya ndege. Pia zinawejengea uwezo madaktari na wauguzi waweze kuhudumia wagonjwa kama wakitokea. Shirika la afya duniani linaendelea kutumia nafasi yake kuisaidia serikali ya Tanzania kuejenga uwezo wa kujiandaa na virusi vya corona COVID19.
MwanaSayansi: Wahudumu katika sekta ya afya wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata au kuwaambukiza wengine ugonjwa huu. Hapa Tanzania, ungewashauri wafanye nini endapo kungetokea maambukizi au mlipuko?
Dkt Saguti:Mlipuko wa homa kali ya mafua ya virusi vya corona unatokana na kirusi aina mpya kabisa. Hivyo Shirika la Afya duniani linaendelea na tafiti zaidi hasa kuhusu jinsi kinavyosambaa
Lakini kulingana na ushahidi wa kitafiti uliopo na kwa kutumia uzoefu uliotokana na virusi aina nyingine ya corona, shirika la afya duniani WHO linashauri wafanyakazi wa afya kutumia njia hizi kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha COVID19.
Kama ilivyo kwa maambukizi mengi ya njia ya hewa, hatua za kwenye mikono na upumuaji zinatumika:
- Nawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka au safisha mikono na kimiminika maalumu cha kuzuia maambukizi
- Funika pua na mdomo ukiwa unakohoa na kupiga chafya kwa kutumia kiwiko cha mkono uliokunja au karatasi ya tishu
- Chukua tahadhari unapohudumia wenye dalili za mafua
Nyongeza, wahudumu wa afya wavae maski wanapoingia kwenye wodi au chumba ambacho kina wagonjwa wanaoshukiwa au waliothibitishwa kuwa na COVID-19.
Unapohudumia wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na COVID-19, kama mhudumu wa afya unatakiwa kuweka umakini kwenye ugunduzi wa mapema, kumtenga mgonjwa haraka na kuzingatia kanuni za kudhibiti kusambaa kwa maambukizi na kutoa tiba zenye viwango.
Kwa wagonjwa wenye dalili mbaya, tiba za kutoa hewa ya oksijeni, kusaidia kupumua kupitia mashine zinhitajika. Matokeo ya tafiti zinazoendelea China yatatupa mwanga kufahamu ugonjwa huu wa COVID-19 kwa undani zaidi.
Shirika la afya duniani limechukua hatua zifuatazo kuhusu wahudumu wa afya.
- WHO inafanya vikao vya mara kwa mara na wataalamu wa afya wanaohudumia wagonjwa wenye COVID-19 ili kufahamu kiundani kuhusu dalili na matibabu.
- Shirika la afya duniani limechapisha muongozo wa matibabu kwa wagonjwa wa COVID-19 wanaohudumiwa hospitalini na ambao wanahudumiwa nyumbani. Pia kuna fomu maalumu ya kumbukumbu ya mgonjwa (standardized clinical case record form – CRF) ambayo ndani ya muda mchache itachapishwa kwenye tovuti ya shirika la afya duniani.
Mpaka sasa hakuna tiba ya COVID19, na matibabu yaliyopo hulenga kutibu dalili za mgonjwa. Mbinu mpya za matibabu zinafanyiwa uchunguzi, pia kupitia tafiti zilizofanyika kwa milipuko ya homa ya corona aina ya MERS-CoV. Shirika la afya duniani linashughurika kuunganisha washirika katika tafiti ili kupata tiba sahihi itakayofanya kazi dunia nzima.
Kwa wale wanaoelewa lugha ya Kiingereza, wanaweza kutazama maswali na majibu kuhusu njia za kujikinga dhidi ya virusi vya corona kwa wahudumu wa sekta ya afya:
MwanaSyansi: Je ni kwa jinsi gani shirika la afya Duniani WHO linafanya kazi kuiwezesha Tanzania kuzuia mlipuko wa virusi vya Corona?
Dkt Saguti: Shirika la afya duniani – WHO linafanya kazi muda wote na wanasayansi, madaktari, wafuatiliaji wa magonjwa, serikali mbalimbali na washirika wasekta binafsi na za umma katika kuunganisha mwitikio wa kupambana na COVID-19 kupitia maeneo mbalimbali ya kitaalamu kama:
- Kusambaza vifaatiba: WHO inasaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata COVID-19 kuwa na uwezo wa kutibu hadi kesi 100. Vifaa hivi vinahusisha maski, gloves, magauni na vifaa vingine vya kuwakinga wafanyakazi wa afya katika nchi 24 amabzo zinachunguza na kutibu wagonjwa wenye COVID19. Maabara 70 zimepatiwa uwezo wa kuchunguza sampuli za wagonjwa wa COVID-19.
- Shirika la afya duniani pia litatumia mfumo maalumu wa usafirishaji (Shipping Fund Programme) ambao ulianzishwa na kitengo cha kufuatilia milipuko ya magonjwa ya mafua ya Infulenza Duniani (Global Influenza Surveillance and Response System) kama njia ya kusafirisha sampuli za wagonjwa wanaohisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
- Chanjo: Shirika la afya duani linafanya kazi na watafiti na wabobezi katika kutafiti upatikanaji wa chanjo na matibabu ya virusi vya corona haraka sana. Tanzania itapewa taarifa kuhusu maendeleo ya tafiti hizi
- Shughuli za kiutawala: Shirika la Afya duniani WHO linafanya vikao vya mara kwa mara na wataalamu wa tiba ambao wanahudumia wagonjwa wa COVID-19 ili kupata taarifa na habari kuhusu ugonjwa huu.
- Kujenga uwezo: Shirika la Afya Duniani limeanzisha darasa la mtandaoni kuhusu elimu ya kugundua, kuzuia na namna ya kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 inapatikana katika tovuti: org.
Shirika la afya duniani- kanda ya Tanzania inafanya kazi na serikali katika maeneo haya:
- Kutoa ushauri :
- WHO inatoa ushauri namna Tanzania inaweza kugundua wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona, namna ya kuwapa tiba wagonjwa na namna ya kuzuia maambukizi kusambaa who.int/health-topics/coronavirus
- WHO imeota ushauri kwa watu namna ya kujikinga wasipate maambukizi , namna ya kuhudumia wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona. Ushauri unajumuisha pia namna ya kujikinga dhidi ya kikohozi, chafya , kunawa mikono na kinga kwenye maeneo yenye mikusanyiko. who.int/health-topics/coronavirus
- WHO imetoa ushauri kuhusu kusafiri na uhusiano na kusambaa kwa maambukizi baina ya mataifa who.int/ith/COVID19_advice_for_international_traffic
- WHO inatoa taarifa za maambukizi ya virusi vya corona kupitia taarifa za moja kwa moja muda wote kupitia tovuti hizi :
- daily situation reports
- WHO Health Emergency dashboard
- WHO COVID19 alerts in African Region
MwanaSayansi: Shirika la Afya duniani kanda ya Afrika limeipa kipaumbele Tanzania, kama miongoni mwa nchi muhimu katika kupambana na virusi vya corona. Kwanini Tanzania imepewa kipaumbele?
Dkt Saguti: WHO inatambua kwamba virusi vya corona vinaleta hali ya hatari zaidi kwa watu na kuna mwingiliano mkubwa wa kibiashara kati ya China, Afrika na nchi nyingine za kiafrika. Kuzingatia hili WHO imezipa kipaumbele nchi 13 za Afrika katika kuzisaidia kwenye mapambano dhidi ya virusi vya corona. Nchini zilizochaguliwa ni pamoja na Tanzania, Algeria, Angola, Cote d’Ivoire, the DRC, the Republic of Congo, Ethiopia, Ghana, Kenya, Mauritius, Nigeria, South Africa, Uganda na Zambia. Kuchaguliwa kwa kumetokana na mwingiliano kati ya nchi hizi na China na nchi nyingine za bara la Asia.
Makala haya yametafsiriwa na Dk Norman Jonas. Kwa mara ya kwanza yalichapishwa katika tovuti ya www.medicopress.media katika lugha ya Kiingereza.