- Tangazo -
Home Maoni ya MwanaSayansi Mtoto akililia wembe mpe, atakuwa mwanasanyansi

Mtoto akililia wembe mpe, atakuwa mwanasanyansi

- Tangazo -

Ilikuwa mchana, baada ya swala adhuhuri, Rehema* na wenziwe waliingia kwenye jengo la kituo cha sayansi Kisosora Tanga wakitoka shule ya jirani. Wote wakiwa wamechafuka kutokana na kucheza mpira baada ya masomo ya darasani, wamebeba vidumu na mifagio.

Nilikuwa kwenye chumba cha maabara, nikiandaa vifaa vya maonesho kwaajili ya ufunguzi wa kituo hichi cha kwanza Tanzania cha sayansi. Kwa sauti ya upole lakini ya kidadisi, Rehema aliniuliza huku akinyoosha vidole kwenye kifaa mezani,”Dokta, hivi hio ni hadubini au darubini?” nilipigwa na butwaa, kwani Rehema ni kijana wa darasa la tano, na anajua kwa majina vifaa vya kisayansi wakati hajawahi kuviona.

Nikampa jani, aweke kwene kioo cha kifaa hicho, atizame na achore anacho kiona. Tangu saa hiyo, kwa furaha, Rehema alikaa ana hadubini hiyo mpaka saa moja usiku, akinyofoa nywele zake, akitafuta wadudu na kuwango’a mbawa na kuviweka chini ya darubini, kuendelea na uchunguzi na kuchora.

Shule za msingi Tanzania hazina maabara, watoto kama Rehema wanajifunza masomo ya sayansi kwa nadharia na kukariri. Wanategemea hasa ustadi wa waalimu wao katika ufundishaji, maana wengi wao wanaona ni magumu na hayaendani na uhalisia wa maisha yao ya kila siku.

Kwa watoto wengi wa umri kati ya miaka 5 hadi 14, wanafundhishwa masomo ya sayansi, hisabati, teknolojia na uhandisi kwa namna ambayo inawapa picha hasi na hofu ya kufeli.

Hata baadhi ya wazazi wanaita hisabati janga la taifa, au baba mkwe. Ufaulu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa tanzania kwa shule za msingi na sekondari umekuwa hafifu ukilinganisha na masomo mengine.

Wakati mwingine hata watoto wanaosoma shule zenye vifaa na rasilimali za kutosha, bado wanapata ugumu katika kujifunza masomo ya sayansi.

Katibu mtendaji wa baraza la mitihani Tanzania, Dkt. Msonde ameripoti kuwa kwa matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kwa mwaka 2020, masomo ya hisabati na sayansi yalikuwa chini ya wastani kwa ujumla.

Tutatizama baadhi ya dhana muhimu katika kuelewa tatizo, na kupata mwanga wa suluhu.

Mtoto anazaliwa akiwa mwanasayansi

Kuna usemi wa kiswahili usemao, mtoto akililia wembe, mpe, akijikata ndipo atajifunza. Mbinu za ki sayansi zinaendana sana na udadisi wa asili wa watoto. Mtoto anapoona wembe, kwake ni dhana mpya, ni sawa na wanasay[1]ansi wanapoona dhana mpya ambayo haijafahamika vema na kuna ombwe la taarifa. Mtoto ana nadharia zake kuhusu wembe na matumizi yake, hajui kama utamkata ama la, vivo hivyo wanasayansi hutunga nadharia kuziba ombwe la taarifa kuhusiana na dhana mpya wanazokutana nazo.

Ukimpa mtoto wembe achezee ni sawa na wanasanyansi wanapofanya majaribio, kuangalia kama nadharia waliotunga ina mashiko katika kuelezea zaidi dhana hio mpya. Wakati wa majaribio, wanasayansi hutizama kwa umakini na kukusanya majibu.

Majibu hayo huwapa taarifa mpya, na taarifa hizo zinaendana na nadharia walioweka mwanzo. Vivo hivyo, mtoto akijikata, atakuwaamejua sasa kuhusu viwembe. Kisha kwa pamoja, watoto na wanasay[1]ansi wanatengeneza hitimisho na kuwa na majibu ya uhakika, na ujuzi mpya unakuwa umetengenezwa.

Dkt Lwidiko ni muasisi wa mradi wa vijana wa Project Inspire anaongoza mabadiliko katika sayansi nchini Tanzania

- Tangazo -
- Tangazo -

Tufuate

570FansLike
330FollowersFollow
100SubscribersSubscribe

Makala Mpya

- Tangazo -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Tangazo -