- Tangazo -
Home Maoni ya MwanaSayansi Dira yetu katika tasnia ya habari Tanzania

Dira yetu katika tasnia ya habari Tanzania

- Tangazo -

MwanaSayansi ni gazeti la Kiswahili linalochapisha habari zitokanazo na maarifa au utafiti wa kisayansi nchini Tanzania na kwingineko duniani. Hili ni chapisho letu la kwanza kabisa.

Tunaanza tukiwa na matarajio makubwa yakuhakikisha taarifa na habari za sayansi, hasa kutoka nchini Tanzania zinapatikana kwa urahisi, kwa Kiswahili na bila gharama kwa msomaji.

Tumejizatiti kutimiza viwango vya juu zaidi vya uandishi wa habari na mawasiliano katika sayansi. La msingi kabisa ni kwamba, tunaanza safari hii tukiwa na nia yakutatua tatizo kubwa katika jamii, ambalo kwa namna moja au nyingine limejidhihirisha hasa wakati wa mlipuko wa janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona(UVIKO-19).

Tatizo hilo ni ukosefu wa taarifa nyeti za kitafiti katika lugha rahisi na kwa Kiswahili. Kwa muda mrefu, pengo hilo lilizibwa na taarifa potofu kutoka kwa watu waliojivika sura ya uanasayansi.

La zaidi nikwamba, katika janga hili, kila mmoja aligeuka mwanadishi wa habari za sayansi, kitu ambacho madhara yake yalijidhihirisha baadae katika jamii, pale ambapo mamlaka zilipata changamoto katika kutekeleza afua kadhaa kukabiliana na janga.

Ni wakati wakuhakikisha taarifa sahihi za kisayansi zinapatikana kwa wote, bila gharama. Tunasema hivi kwasababu mara nyingi tafiti huwekwa kabatini au katika majarida yakisayansi, pengine yale yanayolipiwa, tena yakiwa yameandikwa kwa lugha ya kitaalamu sana.

Hii inazua tatizo katika upatikanaji wa taarifa kwa ustawi wa sayansi kijamii na kiuchumi. Katika hali yakawaida, matokeo ya utafiti yanapaswa kupatikana kwa kila mtu kwa kuwa utafiti mwingi unapaswa kufadhiliwa na serikali na taasisi za umma.

Lakini hii haitokei. Pia, matokeo ya utafiti hayasomwi na umma kwa sababu machapisho mengi hulenga msomaji mtaalam na ni magumu sana kueleweka. Gazeti la MwanaSayansi linaingia sokoni ili kutafsiri matokeo haya ya kisayansi na kuyawasilisha kwa umma kwa urahisi na kwa usahihi. Tunataka kujenga kizazi ambacho kinathamini sayansi na kinaelewea mchango wa sayansi katika kuleta maendeleoa. Tunaongozwa na sheria na kanuni za Tanzania.

Ndiyo maana tunapenda kusisitiza kuwa gazeti hili linathamimi sana haki ya umma yakutafuta, kupata na kusambaza habari, kama ilivyoainishwa chini ya Kifungu cha 18 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Kifungu kinasema kuwa: – “Kila mtu – (a) Ana uhuru wa maoni na maoni ya maoni yake; (b) Ana haki ya kutafuta, kupokea na / au kusambaza habari bila kujali mipaka ya kitaifa; (c) Ana uhuru wa kuwasiliana na uhuru na kinga dhidi ya kuingiliwa na mawasiliano yake; na (d) ana haki ya kufahamishwa wakati wote juu ya hafla muhimu za maisha na shughuli za watu na pia mambo muhimu kwa jamii. ”

Gazeti la MwanaSayansi litajitahidi kutoa habari iliyotafitiwa vizuri, sahihi na isiyo na upendeleo. Tunaahidi kutekeleza jukumu letu kwa uangalifu mkubwa na jukumu la kulinda uaminifu wa umma katika uadilifu wetu.

Katika kuandika habari kutoka kwenye tafiti, daima tutaulizia ushahidi kwa kila madai yanayotolewa na wanasayansi. Ikiwa mwandishi wetu au mhariri atapewa chapisho kutoka kwenye jarida kama ushahidi, tutachunguza zaidi na kuuliza maswali ya msingi: Je, limekidhi vigezo kitafiti?

Tutajitahidi kupata maoni ya wanasayansi wengine wanaoaminika na kutumia mbinu za kukagua ukweli. Tunaamini wewe msomaji utatuunga mkono katika kuitumikia jamii.

- Tangazo -
MwanaSayansi
MwanaSayansihttps://sayansi.medicopress.mediai
MwanaSayansi ni chanzo mahususi cha habari, maoni na uchambuzi kuhusu sayansi na teknolojia nchini Tanzania; hasa katika nyanja ya maendeleo. Taarifa zote na maudhui huzingatia sera na taratibu za MedicoPRESS, asasi iliyoanzishwa kwa lengo la kukuza ujuzi wa waandishi wa habari na wanasayansi katika kuwasilisha taarifa za kitabibu na kisayansi kwa jamii kupitia vyombo vya habari.
- Tangazo -

Tufuate

570FansLike
330FollowersFollow
100SubscribersSubscribe

Makala Mpya

- Tangazo -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Tangazo -