- Tangazo -
Home Maoni ya MwanaSayansi

Maoni ya MwanaSayansi

MwanaSayansi ni gazeti la Kiswahili linalochapisha habari zitokanazo na maarifa au utafiti wa kisayansi nchini Tanzania na kwingineko duniani. Hili ni chapisho letu la kwanza kabisa. Tunaanza tukiwa na matarajio makubwa yakuhakikisha taarifa na habari za sayansi, hasa kutoka nchini...
Huenda wewe ni mmoja kati ya hawa. Ulipata maambukizi ya virusi vya korona na kuugua kwa wiki kadhaa. Ulipata changamoto katika kupumua, homa ikawa juu na kadharika. Kwa bahati nzuri, watoa huduma za afya wakakupigania na ukapata matibabu stahiki,...
Tuanze na maswali 7 ya msingi kuhusu tafiti na uandishi wa habari Tanzania, hasa kwa kuzingatia mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) katika nchi 223 duniani, ikiwemo Tanzania. Je! Kila utafiti uliofanywa na kuchapishwa katika majarida ya...
Kama uko katika mazingira yanayokuweka kwenye hatari ya kupata maambukizi ya vimelea, vikiwemo virusi vya korona au hata bakteria, silaha yako ya kwanza ni kujiweka salama kwa kuzingatia kanuni za afya. Vaa barakoa, nawa mikono kwa sabuni na maji...
Dunia bado inaendelea kushuhudia madhara ya  mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO-19). Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani, watu takribani milioni 104  wameambukizwa na milioni 2.3 wamepoteza maisha tangu ugonjwa ulipotangazwa China mwaka mmoja...
Mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) duniani na hususani barani Afrika, umeleta changamoto nyingi kwenye sekta ya elimu kutokana na zuio la mikusanyiko ya watu.   Dunia imelazimika kugeukia njia za digitali ili kuendeleza shughuli za mwasiliano na...
Hivi karibuni, habari za wanaume hasa wazee kufariki wakiwa faragha na ‘wapenzi wao’ zimeteka vyombo vya habari nchini. Swala hili pia limekuwa sehemu ya mjadala kwenye mitandao ya kijamii na wengi wakilizungumza kwa mzaha. Hatahivyo, huenda kuna wengi bado wanajiuliza:...
Kuna uhitaji wa haraka wa mkakati wa tiba za ugonjwa wa sikoseli (selimundu) barani Africa, hatahivyo, hapa nchini Tanzania kuna mambo kadhaa yakujifunza kuhusu juhudi za uwekezaji katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu. Sikoseli ni ugonjwa unaosababisha seli nyekundu za...
Katika nyakati hizi ambazo mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (uliopewa jina la COVID-19) unazidi kuleta wasiwasi miongoni mwa jamii duniani kote, ni muhimu kuzingatia taarifa zenye ukweli wa kisayansi kuhusu virusi hivyo na njia sahihi za...
Sayansi ya vinasaba (DNA) inazidi kupanuka. Kadri maarifa yanavyoongezeka katika sayansi hii, magonjwa ya kurithi ambayo wanasayansi au jamii walidhani ni ‘magonjwa magumu kueleweka’ sasa yanaweza kutambuliwa kwa ufasaha na kutibiwa katika muda muafaka. Lakini pamoja na hayo, kuna...