Baraza la Kiswahili la Taifa – BAKITA limechapisha istilahi sanifu za Hali ya Hewa, Ugonjwa wa Virusi vya Korona – UVIKO – 19 na Mazingira, kama sehemu ya mfululizo wa warsha tatu za usanifishaji wa maneno ambazo zilifanyika hivi karibuni chini.
Istilahi za hali ya hewa zilisanifishwa mwezi Oktoba 2019, istilahi za UVIKO -19 zikasanifishwa Juni 2020 na zile za Mazingira zilisanifishwa Septemba 2020.
“Istilahi hizi zimekuwa ni msaada mkubwa kwa wadau mbalimbali kwani zimeziba pengo lililokuwapo la uhaba wa visawe vya istilahi katika nyuga zinazohusika,” BAKITA imesema katika chapisho hilo.
BAKITA imeziomba wizara, taasisi na mashirika mengine kutumia fursa hii kuwasilisha istilahi zao ili zikapatiwe visawe vya Kiswahili kwa ajili ya kurahisha mawasiliano kwa umma Taifa.
Kujifahamu istilahi hizo kwa undani: Soma chapisho hapa: