- Tangazo -
Home Afya Je, wajua kuwa vinasaba au DNA huweza kutumika katika tiba yako?

Je, wajua kuwa vinasaba au DNA huweza kutumika katika tiba yako?

- Tangazo -

Sayansi ya vinasaba (DNA) inazidi kupanuka. Kadri maarifa yanavyoongezeka katika sayansi hii, magonjwa ya kurithi ambayo wanasayansi au jamii walidhani ni ‘magonjwa magumu kueleweka’ sasa yanaweza kutambuliwa kwa ufasaha na kutibiwa katika muda muafaka. Lakini pamoja na hayo, kuna muamko zaidi miongoni mwa jamii katika kupenda kufahamu jinsi sayansi ya vinasaba inavyosaidia katika tiba.

Nianze kwa kulielezea hilo nikitumia mifano halisi; hasa katika familia zetu.  Kwa kutumia sayansi ya vinasaba, watu wamepata fursa ya kujua vihatarishi vya magonjwa ya kurithi ndani ya familia zao kwa kutambua ni mwanafamilia yupi mwenye uwezekano mkubwa wa kupata maradhi na nani anaweza kurithisha maradhi hayo kwa kizazi kinachofuata.

Si hilo tu. Kabla mtoto hajazaliwa, watalaamu sasa wanaweza kutabiri uwezekano wa mtoto huyo kupata maradhi ya kurithi kutoka kwa wazazi. Hii ni kupitia upimaji wa vinasaba.

Mfano mzuri ni ugonjwa wa Down’s Syndrome ambao hutokana na kasoro katika chambe za vinasaba au DNA alizorithi mtoto.  Tatizo hili likigunduliwa kabla ya mtoto kuzaliwa, wazazi wanapata nafasi ya kujiandaa na kufanya maamuzi bora kuhusu mustakabli wa mtoto wao.

Je, tunaposema “kasoro’” katika vinasaba tunamaanisha nini?

Kuna wakati mambo yanaweza kwenda ndivyo sivyo na ikatokea hitilafu za kimuundo kwenye vinasaba. Haya ni mabadiliko katia chembe za urithi. Hitilafu hizo huleta kasoro fulani kwenye vinasaba. Hali hii hutambulika kwa lugha ya kitaalamu kama “mutation”

Watu wengi hupenda kujua, je mtu ana kinga dhidi ya kutokea kwa kasoro za kimuundo kwenye vinasaba vyake?

Jibu ni hapana. Kila mtu yupo katika uwezekano wa kutokea kwa kasoro za kimuundo kwenye vinasaba vyake na kasoro hizi hutokana na kurithi kutoka kwa wazazi au sababu za kimazingira, mathalani mionzi ndani ya mwanga wa jua au visababishi vingine vingi.

Sayansi ya vinasaba kwenye tiba huangazia uhusiano uliopo kati ya vinasaba katika mwili wa binadamu na mazingira. Hii husaidia kung’amua uwezekano wa mtu kupata baadhi ya magonjwa na kutoa nafasi kwa wataalamu wa tiba kukinga hatari hiyo ya kutokea ugonjwa.

Sayansi hii ni tawi jipya katika tiba.  Ina nafasi ya kuwa na mchango  mkubwa katika tafiti za saratani, uchunguzi wa magonjwa na uzalishaji dawa na hivyo kuwa yenye manufaa ya moja kwa moja kwenye afya zetu.

Mafanikio yanaonekana, mathalani katika mradi mkubwa wa sayansi ya vinasaba vya binadamu (Human Genomic Project); miongoni mwa miradi ya kibiolojia yenye mafanikio makubwa. Mradi huu uliwakutanisha wanasayansi wa kimataifa na kushirikiana kutafiti mlolongo wa chembe ya urithi au DNA katika miili ya binadamu.

Tunaweza Kujiuliza, je uwekezaji wa mabilioni kama huu una faida gani?

Madhumuni ya mradi huu ilikuwa ni kuzalisha taarifa za kutosha kuhusu vinasaba vya mwanadamu. Taarifa hizi hutumiwa na wanasayansi kutafiti sababu za kibiolojia za magonjwa ya binadamu na kujua namna ya kuyakinga.

Kwa sasa wanasayansi wanatilia mkazo katika kuzichambua taarifa za vinasaba ili zitumike katika kuboresha maisha na kupunguza vifo

.Je wafahamu haya?

Maradhi yasiyoambukiza huweza kuchunguzwa hadi kwenye vinasaba. Hapa, naongelea maradhi ambayo umewahi kuyaona au kuyasikia mfano ugonjwa wa moyo,saratani,magonjwa ya kudumu ya mfumo wa upumuaji.

Kwa kuzingatia sayansi hii ambayo tumekuwa tunazungumzia, tunaweza kupambana vyema dhidi ya magonjwa ya moyo, lehemu iliyozidi na saratani kwa kutumia dawa, lishe na mabadiriko ya mitindo ya maisha hata kabla dalili za ugonjwa hazijaanza.

Tumejifunza kuwa upimaji wa vinasaba una mchango mkubwa kwenye Tiba. Endelea kufuatilia mlolongo wa makala hizi kufahamu jinsi sayansi ya vinasaba inavyoweza kuleta mabadiriko kwenye utoaji tiba kwa mtu binafsi.

Makala haya yameandaliwa na Mohammed Zahir Alimohammed, mtaalam katika biolojia ya vinasaba kutoka Tanzania. Imetafsiriwa kutoka kwenye lugha ya Kiingereza na Dkt Norman Jonas.

- Tangazo -
Avatar
Mohamed Zahirhttp://tshg.or.tz/about-us/
Mohamed Zahir Alimohamed is a trained Molecular Biologist and Biotechnologist. He is currently pursuing a PhD in medical genetics in The Netherlands and Tanzania, studying the use of next generation sequencing in clinical diagnostics of genetic disorders. He is currently a board member of the African Society of Human Genetics, eLife community ambassador 2019 (representing Africa and Europe) and a co-founder and interim secretary general of the Tanzania Society of Human Genetics.
- Tangazo -

Tufuate

570FansLike
330FollowersFollow
100SubscribersSubscribe

Makala Mpya

- Tangazo -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Tangazo -